HabariPilipili FmPilipili FM News

Wavuvi Waonywa Dhidi Ya Mawimbi Mazito Baharini.

Idara ya utabiri wa hali ya anga kanda ya pwani imeonya uwezekano wa kushuhudiwa upepo mkali kuanzia leo hadi Jumamosi.

Upepo huo unatarajiwa kuwa na nguvu zaidi na hatari, na kwamba unatarajiwa kuvuma kwa kasi  ya kilomita 80 kwa saa.

Edward Ngure ambaye ni mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya Mombasa, anasema athari za upepo huo zitashuhudiwa zaidi eneo hili la pwani na hasa katika bahari hindi ambapo huenda mawimbi makubwa yakashuhudiwa.

Ngure amewaonya wavuvi kuwa waangalifu ili kuepuka maafa na hasara na ikiwezekani waondoke baharini pale hali hiyo inaposhuhudiwa.

Sehemu zitakazoathirika zaidi na hali hiyo ni pwani, mashariki mwa nchi, kaskazini magharibi mwa nchi na kaskazini mashariki.

Show More

Related Articles