HabariPilipili FmPilipili FM News

Ada Za Fomu Ya P3 Kupigwa Marufuku Kwale.

Wizara ya afya  kaunti ya Kwale inapanga kupiga marufuku ada za fomu ya P3 zinazotozwa watoto wanaofanyiwa vitendo vya unajisi,  ili kuona kuwa haki za watoto hao zinapatikana  haraka.

Naibu gavana wa kaunti hiyo  Fatuma Achani amesema ada ya shilling 1,500 wanayotozwa waathiriwa , ni ya juu mno na kwamba wazazi wengi hawana uwezo wakulipa ada hiyo.

Achani ameitaja hali hiyo kuchangia  asilimia kubwa ya kesi hizo kunyamaziwa  na kulemaza pakubwa utekelezaji wa haki za watoto.

Show More

Related Articles