HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanamume Afariki Baada Ya Kuanguka Kutoka Juu Ya Mnazi.

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 30 amethibitishwa kufariki baada ya kuanguka kutoka juu ya mnazi.

Charo Kahindi ambaye ni muhudumu wa bodaboda anadaiwa kufariki papo hapo, baada ya kuanguka alipokuwa akiangusha nazi katika maakazi ya maafisa wa polisi mjini Kilifi.

Fred Ochieng ambaye ni kamanda wa polisi kilifi amethibitisha hayo akisema polisi wanaendeleza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Kwa sasa mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali kuu ya Kilifi.

 

Show More

Related Articles