HabariPilipili FmPilipili FM News

Stima Yapotea Mahakamani Wakati Wa Kesi Ya Mkurugenzi Wa Kenya Power.

Maombi  ya dhamana kwa viongozi 14 wa kampuni ya  kusambaza umeme nchini  Kenya Power wanaoshukiwa kuhusika na ufisadi yamekatizwa mapema leo baada ya stima kupotea ghafla mahakamani.

Wanasheria wanaowakilisha washukiwa hao akiwemo Mkurungenzi  mkuu Mtendaji Ken Tarus na Mtangulizi wake Ben Chumo na wengineo walikuwa wanawasilisha hoja zao mbele ya hakimu Mkuu Douglas Ogoti juu ya kwanini watuhumiwa wanapaswa kupewa dhamana kabla ya umeme kupotea.

Hata hivyo mwendesha mashtaka amepinga vikali maombi hayo, akidai washukiwa wanaweza  kuingilia uchunguzi wa kesi hiyo.

Yakijiri hayo tayari waziri wa Kawi Charles Keter kwa ushirikiano wa bodi ya kenya power  amemteua Mhandilisi Jared Otieno kuziba pengo lililoachwa wazi na Tarus.

Show More

Related Articles