HabariPilipili FmPilipili FM News
Dori Amuonya Savula.

Mbunge wa Msambweni kaunti ya kwale Suleiman Dori sasa anamtaka mbunge wa Lugari Ayubu Savula kukoma kuingilia maswala ya miradi inayotekelezwa katika kaunti hiyo.
Hii ni badala ya Savula kutaja Mradi wa kiwanda cha korosho na kile cha sukari cha ramisi kusambaratika, wakati wakaazi wa kaunti hiyo wakisalia kuishi maskwota na wabunge wao wakiyafumbia macho maswala hayo.