HabariPilipili FmPilipili FM News

Kampuni Zaonywa Kutowanyanyasa Wafanyakazi Jomvu.

MBUNGE wa Jomvu Badi Twalib sasa anazitaka kampuni zilizoko eneo hilo kuwa na ushirikiano mwema na wafanyakazi wao.

Mbunge huyo anasema amepokea lalama kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni moja kwamba wanafanyakazi katika mazingira mabaya na kupata malipo duni, hali ambayo ameitaja kuwa kinyume cha sheria za leba humu nchini.

Badi ameapa kupeleka kamati ya leba ya Bunge kwenye kampuni hiyo kuona kwamba wafanyakazi hao wanatendewa haki, akiongeza kuwa jamii ya eneo hilo pia bado haijapata manufaa yoyote kutoka kwa kampuni hiyo.

Show More

Related Articles