HabariPilipili FmPilipili FM News

Mkasa Wa Moto Likoni.

Wakazi wa likoni wamelaani vikali kisa ambapo watu wanne wamefariki eneo la timbwani baada ya nyumba yao kuchomeka usiku wa kuamkia leo.

Baadhi ya wakaazi eneo hilo wamewataka wanandoa kutafuta njia mbadala za kusuluhisha migogoro ya kinyumbani ili kuzuia maafa kama hayo.

Aithibitisha hayo Benjamin Rotich ambaye ni mkuu wa polisi likoni amesema Moto huo ulitokana na mzozo baina ya Mtu na mkewe,kabla ya mwanamume huyo kumwaga petroli na kuichoma nyumba yao.

Amesema waliofariki ni Mkewe mwanamume huyo, na mtoto wake, pamoja na watu wengine wawili kutoka ukoo wa mkewe.

Miili ya wanne hao inahifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali  kuu ya makadara, huku wengine wawili wakiendelea kuuguza majeraha.

Show More

Related Articles