HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ufisadi Kenya Power: Washukiwa 15 kujua Jumanne iwapo wataachiliwa kwa dhamana

Wakurugenzi wakuu 11 katika kampuni ya Kenya Power pamoja na washukiwa wengine wanne wamerejeshwa korokoroni baada ya kufikishwa mahakamani jumatatu adhuhuri kujibu mashtaka dhidi yao kuhusiana na kandarasi ya ununuzi transforma za umeme kwa takriban shilingi bilioni 4.5
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu Dkt. Ben Chumo, mkurugenzi wa sasa Dkt. Ken Tarus pamoja na wasimamizi wa afisi mbalimbali katika kampuni ya Kenya Power wametuhumiwa kushirikiana na watu wengine kutoa zabuni kiholela bila kufutilia utaratibu wa utoaji zabuni, ununuzi wa vifaa ghushi na kutumia njia za udanganyifu kupata malipo kutoka  kwa kampuni ya Kenya Power.
Washukiwa hao walikana mashtaka huku mawakili wa kila mshukiwa akiiomba mahakama kuwaachilia huru kwa dhamana.
Hata hivyo, mahakama ilihairishwa kusikizwa kwa kesi hiyo hadi jumanne asubuhi kuwapa mawakili zaidi nafasi ya kuiomba mahakama washukiwa kuachiliwa kwa dhamana.

Show More

Related Articles