HabariMilele FmSwahili

Mahakama yatoa agizo la kumzuia waziri Yattani kuongoza mikutano ya NSSF

Mahakama kuu imetoa agizo la kumzuia waziri wa leba Ukur Yattani kuongoza mikutano ya bodi ya hazina ya NSSF kufuatia kesi iliyowasilishwa na katibu mkuu wa COTU Francus Atwoli. Jaji Byram Ongaya ametoa agizo hilo baada ya Atwoli kudai kuwa waziri Yattani alifeli kumteua mwakilishi wa COTU katika bodi hiyo Damaris Wanjiru Muhika. Atwoli kupitia wakili Okweh Achiando ametaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria na inayolenga kuwatenga wafanyikazi

Show More

Related Articles