HabariMilele FmSwahili

Serikali yasitisha uhamisho wa vifaru kutoka mbuga za Nairobi na Nakuru

Serikali imesitisha uhamisho wa vifaru kutoka mbuga za Nairobi na Nakuru kufuatia vifo vya vifaru nane weusi katika mbuga ya Tsavo. Katika taarifa waziri wa utalii Najib Balala anasema wanyama hao wamefariki baada ya kunwa maji yenye chumvi. Aidha wataalamu wa mifugo wakiongozwa na profesa Peter Gathumbi wametumwa kuchunguza kiini cha vifaru hao na kuwasilisha ripoti katika juma moja. Waziri amesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya afisa yeyote wa KWS atakayepatikana kuzembea na kuchangia. Vifaru hao ni kati ya 14 walionuiwa kuhamishiwa mbuga hizo ili kuwawezesha kuzaa na kuongeza idadi yao nchini.

Show More

Related Articles