HabariMilele FmSwahili

Rais afanyia mabadiliko uongozi wa kikosi cha Jeshi

Meja jenerali Robert Kariuki Kibochi ndiye naibu mkuu wa majeshi. Kibochi ambaye awali alihudumu kama kamanda wa kikosi cha Kenya Army anachukua mahala pa mtangulizi wake jenerali Joseph Kasaoni ambaye alijiuzulu kwa misingi ya kiafya. Kibochi amekula kiapo chake katika ikulu ya rais Nairobi.
Brigadia wa kwanza wa kike katika kikosi cha KDF, Fatma Ahmed ameandikisha tena historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama meja jenerali wa kikosi cha KDF .Rais Uhuru Kenyatta akimpongeza kwa ujasiri wake

Wengine walioapishwa leo ni Walter raria kamanda wa kikosi cha Kenya Army na Francis Ogola kamanda wa jeshi la angani Kenya Army.

Wakuu hawa wa jeshi sasa wametakiwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuhakikisha taifa linasalia salama wakati wote.

Show More

Related Articles