HabariPilipili FmPilipili FM News

Mazigira Duni Kwa Maafisa Wa polisi Yatajwa Kuathiri Utendakazi Wao.

Mazingira duni ya utendakazi katika Idara ya polisi ukanda wa pwani umetejwa kuzorotesha utoaji wa huduma bora  na uzingatiaji wa haki za binadam

Hatua hiyo inadaiwa kuwapelekea baadhi ya maafisa wa polisi kuhisi kutozingatiwa kwa mahitaji yao  hatua inayochangia ongezeko la ukiukaji wa haki za binadamu  na hata kushidwa kuwahudumia wananchi kikamilifu

Akizungumza katika warsha ya mafunzo kwa maafisa wa polisi katika Gatuzi la Likoni Mombasa, Afisa wa Kitengo cha dharura katika shirika la Muhuri Fahad Changi amehimiza kuzingatiwa kwa haki za binadamu kwa watu wote ikiwemo maafasi wa polisi.

Kwa upande wake mwanaharakati Topister Juma amehimiza ushirikiano wa polisi na mashirika ya kijamii  kuyasaidia makundi ya vijana yanayohangaisha wakaazi

Show More

Related Articles