HabariPilipili FmPilipili FM News

Tatizo La Uhaba Wa Maji Kutatuliwa Mjini Voi.

 

Mkurugenzi wa kampuni ya kusambaza maji mjini Voi Tavevo amewahakikishia wakaazi wa mji huo kwamba hawatakosa maji kwasababu ya deni wanalodaiwa na bodi ya maji ya pwani.

Mkurugenzi huyo Felix Mwarema anasema ukosefu wa maji ambao umeshuhudiwa siku mbili mfululizo  umesababishwa na ukosefu wa dawa ya kusafisha maji ya Chlorine.

Amesema kufikia sasa bodi hiyo imepata dawa hiyo ya kusafisha maji na inaweka mikakati za kuisafirisha hadi Mzima kwa matumizi kabla ya kurejesha huduma zake kwa wakaazi mjini voi na viunga vyake

Show More

Related Articles