
Serikali ina mpango wa kuongeza shule za elimu ya kutwa, ili kupunguza matukio ya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.
Katibu katika wizara ya elimu Dkt Belio Kipsang anasema tayari mpango huu unatekelezwa katika baadhi ya shule ambazo pia ni za bweni.
Hayo yamejiri huku wanafunzi wanne wa shule ya upili ya wavulana ya Homabay wakishtakiwa kwa kujaribu kuchoma shule.