HabariMilele FmSwahili

Visa 39 vya mikasa ya moto shuleni vimeshuhudiwa nchini kufikia sasa

Visa 39 vya mikasa ya moto shuleni vimeshuhudiwa nchini kufikia sasa. Akifika mbele ya wabunge katibu wa elimu Dr Belio Kipsang anasema wanafunzi 142 wamekamatwa kufuatia matukio hayo. Anasema wote hao wanawasaidia maafisa wa usalama na uchunguzi. Aidha anasema wizara hiyo inaunga mkono kuchukuliwa hatua za kisheria wahusika wa matukio hayo.

Kipsang pia amepinga shinikizo la muungano wa KNUT kusitisha zoezi la uhamisho wa walimu wakuu nchini. Amewataka wazazi kushiriki katika kufanikisha zoezi hilo huku akiongeza kuwa wanafunzi kamwe hawataruhusiwa kuwachagua walimu wakuu wa shule zao. Kadhalika ameitaka serikali kuboresha shule za kutwa ili kupunguza idadi ya wanaochagua za mabweni.

Show More

Related Articles