HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanafunzi Watiwa Mbaroni Wakihusishwa Na Uharibifu Wa Mali Shuleni.

Zaidi ya wanafunzi 20 wametiwa mbaroni eneo la Pwani wakihusishwa na uhalifu wa kuteketeza moto mabweni ya shule na kuzua rabsha.

Katika kaunti ya Kisii wanafunzi 8 wa shule ya upili ya wavulana ya Kisii wanazuiliwa rumande baada ya kuteketeza bweni shuleni humo huku shule hiyo ikifungwa kwa mda usiojulikana.

Kufikia sasa, zaidi ya shule 40 zimeathiriwa na misukosuko ya wanafunzi pamoja na uharibifu wa mali, huku serikali ikizidi kuahidi kukaza kamba dhidi ya wanafunzi wanaotekeleza visa hivyo.

Show More

Related Articles