HabariSwahili

Mahakama ya Rufaa yabatilisha uamuzi wa kumng’atua Alfred Keter ,Nandi Hills

Ni afueni kwa  mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter, baada ya mahakama ya rufaa kufutilia mbali uamuzi wa mahakama kuu wa kufutilia mbali uchaguzi wake wa agosti nane mwaka uliopita.
Jaji wa mahakama ya rufaa Erastus Githinji alimpata Keter bila hatia, kinyume na maamuzi ya hapo awali yaliyofutilia mbali uchaguzi wake kwa tuhuma za kuvunja kanuni za uchaguzi.

Show More

Related Articles