HabariMilele FmSwahili

Shule ya upili ya wavulana ya Kisii yafungwa kwa muda usiojulikana

Shule ya upili ya vijana ya Kisii imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia kisa cha bweni kuteketezwa moto usiku wa kuamkia leo. Wanafunzi wote 1, 900 shuleni humo wamemarishwa kuenda nyumbani mara moja. Mkurugenzi wa elimu Nyanza Richard Chepkawai anasema wazazi watajulishwa siku ya kurejea shuleni wanafunzi hao. Tayari wanafunzi 8 wamekamatwa wakihusishwa na kisa hicho baada ya kunakiliwa katika video ya CCTV.

Show More

Related Articles