HabariMilele FmSwahili

Watu 107 waliohusishwa na kisa cha ubakaji Moi Girls waondolewa lawama baada ya uchunguzi wa DNA

Uchunguzi wa DNA umewaondolewa lawama watu 107 waliohusishwa na kisa cha kubakwa mwanafunzi katika shule ya upili ya wasichana ya Moi Girls Nairobi. Mkuu wa kitengo cha jinai Nairobi Nicholus Kamwende ameomba utulivu wakati uhcunguzi huo ukiendelea ili kuwakamata wahusika. Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wakiume katika shule hiyo ni miongoni mwa waliofanyiwa uchunguzi huo wa DNA. Matokeo haya yanawadia siku chache baada ya ripoti ya muungano wa walimu wa sekondari na vyuo anuai KUPPET kudai mwanafunzi husika hakubakwa. Kisa hicho kilitokea tarehe 2 mwezi uliopita na kuchangia kuvunjwa na kubuniwa upya kwa bodi ya shule na mwalimu mkuu kujiuzulu.

Show More

Related Articles