HabariMilele FmSwahili

Matiangi ashurutishwa kuwatimua waliohusika kutoa fidia kwa waathiriwa wa mkasa wa Solai

Waziri wa usalama Dr Fred Matiangi amepewa hadi Jumanne wiki ijayo kuwatimua kazini maafisa wakuu wa serikali walioshirikiana na mmiliki wa bwawa la Patel kutoa fidia kwa waathiriwa wa mkasa huo. Ni kufuatia madai kamishana wa kaunti Joshua Nkatha na maafisa wengine waliwashurutisha wahanga hao kusaini stakabadhi za kuzuia kumshtaki mmiliki huyo. Agizo hilo limetolewa kwa katibu wa utawala katika wizara ya usalama Steven Ole Ntutu baada yake kufika mble ya kamati ya seneti inayochunguza mkasa huo na kudai serikali haikuwa na ufahamu maafisa hao walishirikiana na Perry Mansukh Kansagara kutoa fidia.

Kamati hiyo inayoongozwa na seneta Mutula Kilonzo Jnr inadai huenda maafisa hao wanalenga kuhujumu kesi ya mauaji dhidi ya Manshukh. Aidha kamati hiyo imetishia kuwasilisha kesi mahakamani kushurutisha waathiriwa wa mkasa huo kupewa fidia inayofaa.

Show More

Related Articles