HabariMilele FmSwahili

Serikali kuchunguza madai ya dhulma dhidi ya wafanyikazi wa SGR, Syokimau

Serikali inachunguza madai ya kudhulumiwa wafanyikazi wa Kenya wanaohudumu katika kituo cha reli ya kisasa SGR huko Syokimau. Msemaji wa serikali Erick Kiraithe anasema madai hayo yana uzito ila yameibuliwa kabla ya kuchunguzwa kwa kina. Aidha anasema ni jukumu la kila mfanyikazi katika kituo hicho kuhusika katika uchunguzi ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.

Ametetea muda unaotumika na wanakadarasi hao wa uchina kuendesha mradi huo akitoa hakikisho la kubadilishwa uongozi wake miaka michache ijayo.
Kauli yake inawadia baada ya gazeti mmoja la humu nchini kufichua madhila wanayopitia baadhi ya wafanyikazi raia wa Kenya mikononi mwa wanakadarasi kutoka uchini. Madhila hayo yanahusiana na kunyimwa fursa ya kuabiri magari nyakati za usiku,kutoruhusiwa kukaa meza moja na baadhi ya wachina wanaohudumu katika kituo hicho miongoni mwa mambo mengine.

Show More

Related Articles