HabariPilipili FmPilipili FM News

Maseneta Wamtaka Matian’gi Kuwasimamisha Kazi Maafisa Walioshirikiana Na Wamiliki Wa Bwala La Patel Kuficha Ushahidi

Kamati teule ya seneti inayofanya uchunguzi kuhusiana na mkasa wa Bwawa Patel huko Solai kaunti ya Nakuru, sasa inamtaka waziri wa usalama Fred Matiangi kuwafuta kazi wakuu wa serikali wanaoshirikiana na mmliki wa bwala hilo kutoa pesa kwa wananchi ili wasitoe ushahidi.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati hiyo Mutula Kilonzo Junior kamishna wa kaunti ya Nakuru na manaibu wake wamekuwa wakishirikiana na mmliki wa bwawa hilo kutoa pesa kwa wananchi ili kutoshinikiza kesi dhidi yao, na sasa wanamtaka Matiagi kuwafuta kazi wakuu hao ili kuwa funzo kwa viongozi wengine wa serikali.

Aidha pia seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ameunga mkono kauli hiyo akilaani tukio hilo na kusema ataelekea mahakamani na wakili wake ili kuwatafutia haki waathiriwa wa mkasa huo ulisababisha vifo vya watu 47.

Show More

Related Articles