HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi 8 wa shule ya upili ya Kisii wazuiliwa kufuatia mkasa wa moto shuleni mwao

Polisi wanazuilia wanafunzi 8 wa shule ya upili ya Kisii walionaswa kwenye kamera za CCTV wakiondoka kwenye jumba lililotekelezwa usiku wa kuamkia leo. Haya ni kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Kisii Hassan Abdi anayesmea 8 hao watasaidia katika uchunguzi wao. Naye mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Thurdibuoro huko Kisii ambayo pia bweni lake liliteketea Alex Oyuga anasema wameanzisha uchunguzi kubaini waliohusika na kisa hicho japo akasema huenda wanafunzi hawakuhusika.

Show More

Related Articles