HabariPilipili FmPilipili FM News

Kampeni Ya Kukabili Visa Vya Uchomaji Shule Katika Kaunti Ya Kwale.

 

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imezindua kampeni ya kuvikabili  visa vya  uchomaji wa shule  katika kaunti hiyo vinavyoendelea kushuhudiwa nchini  huku shule ya upili ya wavulana ya Waa, ya Msambweni na ile ya Mwaluphamba  zikiangaziwa kwa ukaribu baada ya majaribio ya kuharibu mali ya shule  mwezi uliopita kungonga mwamba.

Akizungumza  na  wanahabari afisini  mwake  Kamishina wa Kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema kampeni hiyo itawahusisha maafisa wa usalama,wadau mbalimbali  wa  elimu  na wazazi  ili kuona kuwa wanafunzi wanadumisha nidhamu  shuleni.

Ngumo aidha amewataka wanafunzi kukoma kujihusisha na tabia za uharibifu wa mali za shule miongoni mwa nyenginezo kwa kile alichokitaja kuwa serikali inafuatilia kila matukio ya wanafunzi hivyo inaweza kuwaathiri katika maisha yao ya mbeleni wakati wanapotafuta kazi.

Show More

Related Articles