HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kaunti ya Nairobi yatofautiana na wafanyibiashara wa vyoo 

Waendesha biashara ya vyoo jijini Nairobi wamelalamikia kusambaratika kwa biashara yao ambayo wameikuza kwa karibu miongo miwili kutokana na ilani kutoka kwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko akitaka wateja kuvitumia vyoo hivyo bila malipo.

Ilani hiyo ambayo ilifaa kutekelezwa jumapili iliyopita bado inayumbayumba kwani waendesha biashara hiyo wamesimama kidete kwamba hawaondoki wakihofia biashara yao itanyakuliwa na mabwanyenye serikalini.

Show More

Related Articles