HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Elimu Yaagiza Idadi Ya alimu Wanaoshikilia Zamu Katika Shule Za Upili Kuongezwa.

Waziri wa elimu Amina Mohammed ametangaza mikakati mipya ya kupambana na ukosefu wa nidhamu katika shule za upili humu nchini.

Waziri Mohammed ameamuru shule zote za upili za malazi kuongeza idadi ya walimu wanaoshika doria katika muda wa wiki mbili zijazo ikiwemo kuimarisha uangalizi wa vifaa vya wanafunzi  shuleni wakati wanapokuwa madarasani wakidurusu masaa ya jioni.

Amesema zaidi ya wanafunzi 125 kufikia sasa wamekamatwa kwa kuhusishwa na migomo ambayo waziri Mohammed ameitaja kuchangiwa na uoga wa mitihani na ukosefu wa nidhamu.

Show More

Related Articles