HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Mwakirunge Walalamikia Kuwepo Kwa Jaa La Takataka Katila Eneo hilo

Wakaazi wa Mwakirunge eneo bunge la Kisauni hii leo wameandamana wakilalamikia mikurupuko ya maradhi na kufungika kwa barabara kutokana na jaa la takataka  lililoko eneo hilo.

Wakiongozwa na Shabani Salim waakazi hao wanasema jaa hilo limewaletea magogwa ya kipindukipindu pamoja na kufungika kwa barabara na sasa wanamuomba Gavana Hassan Joho na serikali yake kuingilia kati ili kuhakikisha taka hizo haziendelei kuleta madhara zaidi na ikiwezekana kuondolewa kwa jaa hilo kabisa.

Taka hizo zinadaiwa kutolewa katika jaa la kibarani ambalo lilifungwa hivi majuzi.

Show More

Related Articles