People Daily

Maafisa Wa KRA Waliohusika Na Uuzaji Wa Ethanol Wasimamishwa Kazi.

Mamlaka ya ushuru nchini KRA imewasimamisha kazi maafisa wake watatu wanaodaiwa kuhusika na uuzaji wa kemikali ya Ethanol iliyopangiwa kuharibiwa huku ikisubiri uchunguzi kufanywa.

Maafisa hao ambao ni wa hapa Mombasa, wanadaiwa kuchagia uuzaji wa shehena 8 za ethanol kinyume na zoezi la mnada wa kawaida linalofanywa na KRA.

Shehena hizo nane zilipangiwa kupigwa mnada mnamo mwaka 2016.

KRA kupitia taarifa yake inasema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya maafisa wake kwa hatia ya kuuza kemikali hiyo ya Ethanol.

Show More

Related Articles