HabariPilipili FmPilipili FM News

Watoto Wanaoishi Na Ulemavu Kunufaika Na Mradi Wa KIDS CARE.

Watoto wanaoishi na ulemavu kaunti ya kwale wamepangiwa kufaidi na mradi unaoendeshwa na shirika moja la kijamii la KIDS CARE, kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hiyo.

Ali Mwaziro aliye mkurugenzi wa shirika hilo anasema mradi huo chini ya kauli mbiu ‘YES WE CAN’ unalenga zaidi sehemu za lungalunga, ambazo zimetajwa kuandikisha idadi kubwa ya watoto wanaoishi na ulemavu wa akili na hata ule wa kimwili, kuona kuwa watoto hao wanapata huduma bora za afya na elimu.

Ramadhan Masood Bungale  ambaye ni katibu wa huduma za kijamii kaunti ya kwale ameeleza kuwepo mipango ya kaunti hiyo kusaidia watoto hao, akisema tayari wamesajili watoto wapatao 3,817, ambapo 1,700 kati yao ni kutoka eneo la lunga lunga.

Bungale amesisitiza haja ya wananchi kuhamasishwa zaidi dhidi ya unyanyapaa kuhakikisha watoto hao wanapata mazingira bora

Show More

Related Articles