HabariMilele FmSwahili

Matiangi : Huenda bidhaa za magendo zilizonaswa nchini zikachukua muda kabla ya kuteketezwa

Huenda bidhaa za magendo zilizonaswa nchini zikachukua muda kabla ya kuteketezwa. Waziri wa usalama Fred Matiang anasema zoezi hilo linachelewa kutokana na kwamba lazima mahakama itoe kibali. Matiangi anayefika mbele ya kamati ya usalama bungeni anasema bidhaa za mamilioni ya pesa zilizoingizwa nchini kimagendo na ambazo ni hatari kwa matumizi ya binadamu zimenaswa kufikia sasa zikiwemo sukari, mbolea na mahindi na zitateketezwa karibuni.

Show More

Related Articles