HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Mombasa Walalamikia Uhaba Wa Maji.

Hisia mseto zinaendelea kuibuka miongoni mwa wananchi kaunti ya mombasa kuhusiana na tatizo sugu la uhaba wa maji.

Wengi wa wananchi kutoka mitaa mbalimbali ya kaunti wamedai kukosa maji safi ya mfereji kwa zaidi ya miezi miwili, hali ambayo imewalazimu kuishia kutumia maji ya visima.

Kwa wale wanaonunua maji safi ya mfereji wamedai kununua mtungi mmoja wa maji kati ya shilingi 50 na 70.

Wameitaka serikali ya kaunti na bodi ya maji pwani kuingilia kati suala hilo kuona kuwa wananchi wanapata bidhaa hiyo.

Show More

Related Articles