People Daily

Shughli Za Masomo Za Tatizika Kwa Siku Ya Pili Katika Shule Ya Upili Ya Majaoni Kaunti Ya Kilifi.

Shughuli za masomo zimekwama kwa siku ya pili mfululizo katika shule ya upili ya Majaoni Kaunti ya Kilifi, baada ya walimu kususia kazi kwa madai ya kunyanyaswa na mwalimu mkuu pamoja na bodi ya shule hiyo.

Walimu hao wamedai mwalimu huyo Sarah Mwawato amekuwa akishirikiana na bodi ya shule kufuja pesa, na kuwatishia kuwafuta kazi walimu watakao enda kinyume na matakwa yao. Sasa wanataka mwalimu huyo aondolewe  mara moja, na bodi simamizi ya shule hiyo ivunjiliwe mbali la sivyo wapewe uhamisho.

Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Tezo Thomas Chengo ameitaka Tume ya kuajiri walimu nchini TSC kuchukua hatua za dharua dhidi ya tatizo hilo ili kuzuia wanafunzi kuendelea kuathirika kimasomo.

Charles Magunda ambaye ni katibu mkuu wa muungano wa walimu wa shule za upili eneo hilo amesema tayari mikakati imewekwa kuona kuwa shughuli za masomo zinarejea hali yake ya kawaida

Show More

Related Articles