HabariSwahili

Mpaka mpya kati ya Kenya na Tanzania wazua taharuki

Taharuki  imetanda miongoni mwa raia  wa Kenya  na Tanzania  wanaoishi kwenye  eneo la mpaka , huku baadhi ya wananchi wakipoteza ardhi  yao kwa nchi jirani na wengine hata makaazi, kufuatia kuwekwa upya kwa  mpya kati ya nchi hizo mbili  .
Wenyeji wanasema kuwa wengine wamepata ardhi yao ikiwa Kenya , na nyumba zao zikiwa Tanzania , nayo serikali  ya Kenya ikisisitiza kuwa  hakuna fidia  itatolewa kwa wale waliopoteza ardhi yao, kwani walifahamu fika kuwa waliwekeza kwenye eneo la mpaka.
Marais Uhuru Kenyatta na Pombe Magufuli wanatarajiwa kuzindua rasmi mpaka huo mwishoni mwa wiki.

Show More

Related Articles