HabariSwahili

Wafanya biashara Waandamana jijini kulalamikia kuzuiliwa kwa mizigo yao Mombasa

Mamia ya wafanyabiashara walitatiza shughuli kati kati mwa jiji la Nairobi kwa kufanya maandamano ya kulalamikia kuzuiliwa kwa mizigo yao bandarini Mombasa kwa muda wa miezi sita sasa.
Hali hiyo imesababishwa na msururu wa misako dhidi ya bidhaa ghushi ambao umekuwa ukiendelea nchini.
Athiri zake sasa zimewasababishia hasara kubwa  wafanyabiashara wadogo wanaohusika katika biashara ya kununua bidhaa nje ya nchi na kuziuza hapa nchini.

Show More

Related Articles