BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Kenya bixa yatia saina mkataba Wa Maelewano na Benki Ya KCB

 

Usimamizi wa kampuni ya kenya bixa kaunti ya kwale umetia saini mkataba wa maelewano na benki ya KCB hii leo ili kuona kuwa zaidi ya wakulima 6000 wa mrangi wa bixa kwale wananufaika na mikopo kutoka kwa benki hio ili kuimarisha kilimo hicho.

Kampuni hiyo ya mrangi iko katika harakati za kufufua kilimo cha mmea huo kilichosambaratika miaka ya tisini, kwa kuwaelimisha na kusajili wakulima ili kupata malighafi itakayopelekea kiwanda hicho kuanza kazi.

Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo katika afisi za kampuni hio meneja mkuu wa Kenya Bixa David Kisa amesema ushirikiano na KCB utawainuia wakulima kimaisha kinyume na ilivyokua  hapo awali akiwataka wakulima hao kukitilia maanani kilimo hicho kwa manufaa yao.

Kwa upande wake meneja KCB katika  kitengo cha MobiGrow  Dickson Naftali amesema kua watapeana mikopo hadi ya Sh100,000 kwa wakulima  ila itategemea  na uwezo na makubaliano baina ya wakulima na benki hio kwani wanaezapata hata zaidi ya mkopo huo.

Show More

Related Articles