HabariMilele FmSwahili

EACC kuchunguza mali wanazomiliki Swazuri na Abigael Mbagaya

Tume ya ufisadi inachunguza mali wanazomiliki mwenyekiti wa tume ya ardhi Mohammed Swazuri na naibu wake Abigael Mbagaya. Hii ni baada ya tume hiyo kukabidhiwa rekodi za mali walizokuwa wakimiliki kabla ya kuingia afisini hadi kufikia sasa. Swazuri na Mbagaya ni baadhi ya makamishan wa tume ya ardhi ambao wanachunguzwa kwa kutoa fidia maradufu kwa walioathirika na ujenzi wa reli ya kisasa SGR. Kadhaika Swazuri na kundi lake wamehusishwa na sakata ya ardhi ya Ruaraka.

Show More

Related Articles