HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu 9 Wadhibitishwa Kufariki Katika Ajali Mbaya Ya Barabarani.

Watu 10 hawajulikani waliko kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo, katika barabara kuu ya mombasa Nairobi.

Samuel Kimaru ambaye ni kamanda mkuu wa idara ya trafiki anasema basi la kampuni ya Bascar lililohusika kwenye ajali eneo la Sultan Hamud, lilikuwa na abiria 39 wakati wa ajali hiyo ambapo watu 9 wamethibitishwa kufariki, huku 20 wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kilome, na wengine 10 wakiwa hawajulikani waliko.

Kimaru amehusisha ajali hiyo na utepetevu wa madereva akiwataka kuwa makini barabarani usiku na mchana hasa wakati huu ambapo mvua inaendelea kunyesha.

Kulingana na Kimaru Jumla ya watu 1,521 wamefariki kwenye ajali tangu mwaka huu kuanza wengi wao wakiwa wapita njia na abiria.

Show More

Related Articles