HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi aliyepotea wa shule ya wasichana ya Ngara apatikana mjini Mombasa

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kupatikana kwa mwanafunzi wa miaka 16 wa shule ya upili ya wasichana ya Ngara aliyepatikana mjini Mombasa. OCPD wa kituo cha Central mjini Mombasa Eliud Arumba anasema polisi wanawasaka watu waliomsafirisha Kadhalika amesema msichana huyo amewaambia polisi kuwa kulikuwepo na mgogoro baina yake na wazazi wake kabla ya kutoweka kwake juma moja lililopita.

Show More

Related Articles