HabariMilele FmSwahili

Wafanyibiashara jijini Nairobi waandamana kushinikiza maslahi yao kuangaziwa

Wafanyibiashara hapa jijini Nairobi wanaandamana wakati huu kushinikiza maslahi yao kuangaziwa. Kati ya mengine wafanyikazi hao wanamtaka gavana Mike Sonko kupunguza gharama ya leseni. Pia wanasema askari wa kaunti wamekuwa wakiwahangaisha na kuhujumu biashara zao.
Wakati huo huo madereva wa magari ya teksi yanayohudumu kupitia mtandao wameendelea kugoma wakilalamikia kile wanadai ni kushurutishwa kulipisha nauli ya chini. Madereva hao walioanza mgomo wao Jumatatu wiki hii wanasema hawatarejea kazini hadi wizara ya uchukuzi iingilie kati suala hilo.

Show More

Related Articles