HabariPilipili FmPilipili FM News

Tani 40,000 Za Sukari Zazuiliwa Katika Bandari Kuu Ya Mombasa.

Takriban tani 40,000 za sukari bado zipo katika meli moja inayodaiwa  kutia nanga katika bandari ya mombasa miezi 10 iliyopita.

Meneja mkuu wa bandari ya KPA captain William Ruto amesema meli hiyo ilinyimwa ruhusa ya kupakua mzigo huo.

Haya yanajiri  siku chache baada ya taarifa kufichuka kuhusu meli moja, ambayo inadaiwa kupotelea katika bahari hindi ikiwa imebeba tani elfu 10 za mbolea,kwa kuhofia kuwa mbolea hiyo ingenaswa katika msako unaoendelwa wa kukabiliana na walanguzi wa bidhaa ghushi nchini.

Meli hiyo ilikuwa inatokea Morrocco ikileta mbolea hiyo katika bandari ya mombasa.

Show More

Related Articles