HabariPilipili FmPilipili FM News

Mkrugenzi Wa Mashtaka Ya Umma Aagiza Gavana Wa Busia Atiwe Mbaroni.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajj ameagiza kukamatwa kwa gavana wa Busia Sospeter Ojamong.

Gavana Ojamong na maafisa wengine 8 wa kaunti hiyo wanakabiliwa na tuhuma za kutoa tenda kwa njia ya ufisadi, ambapo shilingi milioni 20 zinadaiwa kufujwa.

Wote hao pia wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya afisi na pia kukiuka sheria za ununuzi wa mali ya umma.

Kati ya maafisa hao ni pamoja na Timon Otieno, Bernad Krade Yaite, Lenard Wanda, Samuel Osieko na Allan Omachari. Wengine ni Edna Adhiambo Odoyo, Ranish Achieng pamoja na Sebastian Hallens.

Hajji ansema upo ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka maafisa hao 9 wa kanti ya Busia.

Show More

Related Articles