HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa 6 Wa Uhalifu Wasakwa Kisauni.

Polisi wanaendesha oparesheni ya kiusalama eneobunge la kisauni hapa mombasa kuwasaka vijana wanaoaminika kutekeleza visa vya uhalifu eneo hilo.

Haya yanajiri siku moja baada ya kijana mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi, pale alipojaribu kuwashambulia maafisa hao kwa panga.

Akithibitisha hayo kamanda wa polisi eneo hilo Sangura Musee anasema kijana huyo alipigwa risasi baada ya kujaribu kushambulia polisi kwa upanga.

Musee amesema msako unaendelea kuwatafuta vijana 6 zaidi waliokuwa pamoja na kijana huyo, na ambao walifanikiwa kutoroka

Show More

Related Articles