HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanamume Mmoja Apatikana Kama Amefariki Baharini.

Mwili wa mwanamume mmoja umepatikana ukielea baharini eneo la Tamarind karibu na bandari ya Zamani   eneo la Nyali hapa Mombasa.

Mkuu wa Kitengo cha maafisa wa ukaguzi wa kaunti Mohamed Amir amesema wamepata taarifa kuhusu kisa hicho kutoka kwa watu wawili waliokuwa wakiogelea eneo hilo.

Amir anasema wamefanikiwa kuutoa mwili huo na kuupeleka katika chumba cha maiti katika hospitali ya kadara, akiongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini kilicho sababisha kifo cha jamaa huyo.

Kulingana na Amir hiki ni kisa cha pili kwa muda wa miezi miwili sasa. Amehimiza wakazi na wageni wanaozuru eneo hilo kusalia wangalifu wakati wakiogelea baharini ili kuepuka maafa zaidi.

Show More

Related Articles