HabariMilele FmSwahili

Wahudumu wa texi za Uber ,Taxify na Little ride waandamana kulalamikia malipo duni

Mamia ya wahudumu wa texi zinazotumia mitandao yaani Uber,Taxify na Little ride wameandamana hapa Nairobi kulalamikia malipo duni. Wakiongozwa na mwenyekiti wao David Muteru wanasema wamepata hasara kutokana na hatua ya kampuni hizo kupunguza nauli. Wameitaka wizara ya uchukuzi kuingilia kati huku wakiapa kususia kazi hadi swala hilo litatuliwe.

Nao wahudumu wa boda boda wameandana kulalamikia kuhangaishwa wakiwa kazini. Wahudumu hao wanasema piki piki zao zimekuwa zikinaswa kinyume na sheria huku wakiendelea kupinga agizo kwao kutohudumu kati kati ya jiji.

Show More

Related Articles