HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughli Za Uchukuzi Kuimarika Zaidi Katika Eneo la Pwani.

Huenda uchukuzi ukaimarika pakubwa kufuatia mikakati inayotekelezwa na Idara ya trafiki kanda ya pwani.

Kati ya mikakati hiyo inahusisha kuondolewa vizuizi vyote vya barabarani hasa katika barabara kuu ya mombasa kuelekea malaba.

Hayo ni kwa mujibu wa kamanda wa polisi eneo hili la pwani Noah Mwivanda, ambaye anasema vizuizi vya barabarani vitawekwa tu pale kuna msako maalum wa kuwasaka wahalifu.

Kulingana naye agizo hilo lilianza kutekelezwa wiki mbili zilizopita ili kuzuia kutatiza shughuli za uchukuzi katika barabara kuu eneo hili.

Show More

Related Articles