HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Kuekeza Kwa Vyuo Vya Kiufundi Katika Kila Eneo Bunge.

Ni afueni sasa kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya kiufundi humu nchini.
Hii ni baada ya serikali kupunguza karibu nusu ya ada za vyuo hivyo ikiwemo kutenga basari ya shilingi elfu 30 kwa kila mwanafunzi atakaye jiunga na vyuo hivyo kuanzia mwezi wa septemba.
Mpango huo unalenga kuvutia wanafunzi wengi kuchukua kozi za kiufundi.
Naibu rais William Ruto anasema mpango huo pamoja na ule wa mikopo ya elimu ya ngazi ya juu unalenga pia kuhakikisha wanaotaka kufanya kozi za kiufundi wanafanya hivyo bila kusumbuka, akiongeza kuwa serikali inawekeza kwa vyuo vya kiufundi katika kila eneo bunge kuona kuwa vijana wanapewa ujuzi wa kuwasaidia kujikimu kimaisha.

Show More

Related Articles