HabariMilele FmSwahili

Gavana Sonko azindua mpango wa elimu ya chekechea bila malipo

Gavana wa Nairobi Mike Sonko leo amezindua mpango wa elimu ya chekechea bila malipo kaunti hii. Akizungumza wakati wa kuzindua mpango huo Sonko amesema idadi kubwa ya watoto wamekosa kujiunga na masomo ya chekehckea kutokana na karo ya juu ambayo wamekua wakilipishwa akisema mpango huu utakuwa ni afueni kwa wazazi, na pia kuimarisha kiwango cha watoto wanaojiunga na chekechea. Chin ya mpango huu kila mwanafunzi wa chekechea atalipiswa shilingi 3,815 na kaunti hii. Anasema kuwa kaunti pia inalenga kuwaajiri walimu 500 zaiid wa chekechea kufanikisha mpango huu.

Show More

Related Articles