HabariMilele FmSwahili

Rais akutana na kushauriana na ujumbe wa viongozi kutoka Marekani

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na kushauriana na ujumbe wa viongozi kutoka Marekani kaitka ikulu ya Nairobi hivi leo. Ujumbe huo umeongozwa na katibu mkuu wa biashara ya kimataifa wa serikali yamarekani Gil Kaplan, mazungumzo baina yao yakiangazia zaidi masuala ya biashara na uekezaji baina ya Kenya na Marekani. Mkutano wa leo umekujia wakati Kenya ikijiandaa kutuma ujumbe wa viongozi Marekani, kuipigia taifa hili upatu kama moja wapo ya mataifa bora kufanya biashara. Pia ziara hiyo inakujia Kenya ikijiandaa kufanya safari ya kwanza ya moja kwa moja hadi Marekani Oktoba mwaka huu. Pia walijadili kuhusiana na kujengwa barabara kuu ya kisasa kutoka Mombsa hadi Nairobi, mradi utakaoendeshwa na kampuni moja ya Marekni. Pia walijadili mkataba baina serikali na marekani kuhus utekelezwaji wa agenda nne kuu za rais.

Show More

Related Articles