HabariMilele FmSwahili

Rais atia saini mswada wa matumizi ya fedha za serikali

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini mswada wa matumizi ya fedha za serikali hatua inayoruhusu matumizi ya shilingi trilioni 1.4 kuwafikishia wananchi bidhaa na huduma mbali mbali. Kiasi hiki ni kando na shilingi bilioni 398.5 zitakazokusanywa kufadhili matumizi ya serikali. Kwa ujumla serikali kuu imetengewa shilingi trilioni 1.6 katika bajeti ya mwaka ujao wa kifedha 2018/2019. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 17.2 zitatolewa kama mikopo kwa serikali za kaunti. Kaunti zimeratibiwa kutumia shilingi bilioni 9.4 kukodisha vifaa vya matibabu, shilingi bilioni 4.3 zikitengewa hospitali za level 5, shilingi bilioni 2 zitatumika kukarabati vyuo vya anuai.

Show More

Related Articles