HabariMilele FmSwahili

Wizara ya kilimo yaanzisha mikakati ya kufufua viwanda vya sukari nchini

Wizara ya kilimo imesaini mkataba na viongozi wa maeneo yanayosaga sukari utakaoruhusu kubuniwa jopo la kuangazia jinsi ya kufufua viwanda vya sukari vilivyositisha shuguli zao. Waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri anasema jopo hilo litapendekeza jinsi ya kukifufua kiwanda cha Mumias,namna viwanda vya sukari vitanunua miwa kutoka kwa wakulima pasi na ushindani usiostahili na kupata wafadhili kusaidia viwanda vilivyositisha shuguli zake. Kiunjuri anasema wameafikiana mataifa yalio wanachama wa COMESA pekee kuruhusu kuingiza sukari nchini ili kuepuka uagizaji wa sukari utakaoathiri kampuni za humu nchini na pia utoaji leseni kwa viwanda vya sukari kufanywa kupitia mashauriano ya serikali kuu na kaunti na wadau wote.

Show More

Related Articles